Mvua yakata mawasiliano ya miundombinu ya barabara Rungwe, Mbeya
17 April 2024, 12:12
Katika hali isiyotarajiwa wakazi wa kata ya Kapugi na Lyenje wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wamekutana na adha ya kuharibika kwa miundombinu ya barabara iliyokuwa ikiwaunganisha na kusababisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kusimama.
Na Ezra Mwilwa
Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha barabara ya Kapugi-Lyenje Ikuti kupitia mto Kiwira kuharibika na hivyo kuondoa mawasiliano kati ya vijiji hivi viwili.
Mbunge wa jimbo la Rungwe Mhe. Anton Mwantona amefika katika eneo la tukio na kukagua madhara yaliyojitokeza na amewaomba wakazi wa wilaya ya Rungwe kuendelea kuchukua tahadhari dhidi majanga katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha nchi nzima.
Mbunge Mwantona amewataka wananchi wa vijiji hivyo kuwa watulivu kwenye kipindi hiki kigumu kwani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atafanya kama alivyowapa barabara mwanzoni waamini hata sasa hawezi kuwsacha wapate shida kwa sababu anawapenda wananchi wa Kapugi, Lyenje na Ikuti.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rungwe komrade Mwakipunga amefika katika eneo la tukio na kuwapa pole wananchi wa kata Kapugi na Lyenje kwa kuharibikiwa na miundombinu ya barabara hiyo.
Nao baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo wakiongozwa na Diwani wao Mhe. Abraham Kapange wamemshukuru Mbunge na chama kwa kufika katika eneo la tukio na kuwafariji.