Wachungaji kemeeni mambo ya ushoga unaoendelea duniani
8 April 2024, 20:02
“Tumieni elimu na maarifa mliyoyapata vyuoni kuuaminisha ulimwengu juu ya imani ya kumtegemea Mungu na siyo fedha.”
Na Ezra Mwilwa
Wachungaji waliopo masomoni Chuo Kikuu Teofilo Kisanji na Chuo cha Itengule Mbeya wametakiwa kuendelea kukemea maswala ya ushoga yanayoendelea duniani.
Wito huo umetolewa na Kasisi wa kanisa la Angilikan Dayosisi ya Southern Canon Isac Mbwaga katika Chuo cha Utengule wakati akiwasilisha mada iliyokuwa imelenga kuwajenga wachungaji wanafunzi kufundisha kweli juu ya mambo ya ushoga.
Nao baadhi ya wathiolojia walioshiriki katika mdahalo huo wamesema kama wachungaji wasiogope kusema kweli na kufundisha watoto walio shuleni na maeneo mbalimbali.
Kwa upande wao wachungaji Mhadhiri na Mchungaji wa Ushirika wa Teku Ekisa Shibanda na Makamu wa chuo cha Utengule mchungaji Tulinagwe Kibona wamesema ni vyema kila mtumishi anapopata nafasi ya kufundisha mahali popote aendelee kukemea suala la ushoga.