Madaktari bigwa kuweka kambi Mbeya,wananchi kunufaika
4 April 2024, 10:17
Unapokuwa na afya njema inakupa kuwa na mwendelezo wa kutimiza majukumu yako ikiwemo yale ya kiuchumi na yakijamii.
Na Ezra Mwilwa
Hospital ya Rufaa kanda ya Mbeya Imeandaa kambi maalumu ya upasuaji wa Ubongo, Uti wa mgongo na Mishipa ya Damu kwakushirikiana na wataalamu kutoka Hospital ya Moi.
Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi wa hospital ya Rufaa kanda ya Mbeya Daktari Godleve Mbwanji amesema kambi hiyo itaanza tarehe 8 hadi tarehe 12 Mwezi April 2024.
Ameongeza kuwa katika kipindi chote cha kambi hiyo wananchi wanakaribishwa kwenda kupata matibabu ya matatizo hayo katika kipindi cha kambi hiyo na baada ya kambi hiyo huduma hiyo itaendelea kutolewa.
Nae Daktari Bigwa wa magojwa ya Mishipa ya fahamu, Ubongo na Uti wa mgongo Dkt. Boniface Kivevele amesema katika kipindi chote watakacho kua na wataalamu kutoka Hospital ya Taifa Mhimbiri watajikita na Magojwa ya mfumo wa Fahamu na Magonjwa ya watoto wadogo walio zaliwa nayo.