Aliyekuwa kamanda wa polisi Songwe awaaga waandishi wa habari
21 March 2024, 19:16
Unapofanya kazi mahali wapo watu unawakuta na unapokelewa na kupewa ushrikiano,basi iko hivyo unapoondoka pia ni vyema kuaga .Hii inatufundisha kutoka kwa SAPC. Theopista Mallya ambaye ameona umhimu wa kuwaaga baadhi ya watu ambao amefanya kazi nao katika mkoa wa Songwe.
Na mwandishi wetu
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SAPC. Theopista Mallya ambae amepangiwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ambapo ameeleza namna alivyofanya kazi na waandishi wa habari mkoani humo na kuonesha ushirikiano mkubwa katika kipindi chote alichohudumu katika mkoa wa songwe.
Hayo yamejiri wakati wa kikao cha pamoja kati ya waandishi wa habari, Jeshi la Polisi na wadau mbalimbali Mkoani Songwe kilichofanyika katika ukumbi wa Mpende Jirani Wilayani Mbozi ambapo kimejadili utekelezaji wa maazimio mbalimbali pamoja na kuunda kamati ndogo ya Mkoa kwa ajili ya ufuatiliaji wa madhara wanayopata waandishi wawapo kazi.
Katika kikao hicho SAPC Mallya alitumia nafasi hiyo kuwaaga waandishi wa habari kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanywa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP. Camillus Wambura
“Nachukua fursa hii kuwaaga baada ya kupangiwa kuwa Kamanda wa mkoa wa Dodoma hivyo basi nawashukuru sana wananchi wote wa mkoa wa Songwe namna walivyonipa ushirikiano ambapo ulifanya kazi za polisi kwangu kuwa rahisi na kupelekea Mkoa huu kuwa miongoni mwa Mikoa ambayo iko swali na uhalifu ulishuka kwa kiasi kikubwa hata hivyo elimu tuliokuwa tunatoa kupitia mashuleni makanisani misikitini hasa kwenye maswala ya ukatili yakiwemo ulawiti kwa watoto ulipungua kwa kiasi kikubwa sana Kutokana na ushirikiano ambao nilikuwa napewa na kama mlivyosema kwamba atakaye kuja basi nimueleze kuwa nini wananchi wa songwe wanataka ili aweze kwenda nao sawa kwani ukiwapa watu ushirikiano, ukiwa muwazi basi watakupa ushirikiano mkubwa sana wa kuweza kufanya kazi kwa urahisi sana lakini pia waandishi wa habari ninawashukuru sana sana kama sio ninyi mimi nisingeweza kufanya yale ambao nimefanya na kuwafikia wananchi ni elimu ambao ilisaidia sana kufanya wananchi wa mkoa wa Songwe kutuelewa sisi polisi na kuelewa kuwa polisi sio adui bali ni rafiki ambaye anawafanya waishi kwa usalama Kwa sababu bila usalama hakuna maendeleo.“amesema SAPC Mallya