Kyandomo ahimiza wanawake kugombea nafasi za uongozi
12 March 2024, 21:35
Suala la uchaguzi limekuwa ni suala la kila mwananchi kushiriki ingawa katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi baadhi ya makundi yamekuwa na idadi ndogo ya wagombea ikiwemo kundi la wanawake.
Na mwandishi wetu
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhe. Suma Fyandomo amewataka wanawake kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozikwani uwezo wanao na hawashindwi kutekeleza majukumu mbalimbali ya Kifamilia, Kijamii na kitaifa kwa ujumla huku akisistiza kuondoa hofu wakati wa kutina ya kufanya jambo lolote
Kauli hiyo ameitoa akiwa kwenye ziara maalumu iliyofanyika katika viwanja vya Msifuni kijiji cha Ifuma kata ya Lupa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
”Wanawake niwatie moyo kwenye nafasi zozote zinapojitokeza msisite, msiogope mnatakiwa kusonga mbele kuwa mstari wa kwanza kwenda kuchukua fomu au kuomba nafasi hizo kwasababu wanawake tunaamini hatushindwi , wanawake ni Jeshi kubwa lakini pia ni nguzo kubwa ya familia”amesema Mhe. Fyandomo.
Aidha Fyandomo ameongeza kuwa wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza mbele yao akisema ujasiri ndio iwe nguvu ya kuchangamkia fursa hizo kwani uwezo wanao na wanaweza hata wasipowezeshwa huku akirejerea uwezo wa wanawake kukabili majukumu ya Familia zao pindi wakinababa wanapotelekeza familia zao.