Viongozi wa dini Mbeya kuadhimisha maridhiano day kwa kufanya kazi za kijamii
15 February 2024, 15:37
Na Hobokela Lwinga
Kuelekea katika kilele cha siku ya maridhiano nchini ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika mkoani mbeya,viongozi wadini wameanza kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo upandaji miti,uchangiaji wa damu pamoja na utoaji elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Akizungumza katika uzinduzi wa kutekeleza shughuli hizo katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa wa mbeya kati ya viongozi wa dini na wandishi wa habari,mkuu wa mkoa wa mbeya Juma Zuberi Homera amesema katika kilele cha maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajia kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Aidha Homera amesema katika kabla ya maadhimisho hayo zipo shughuli mbalimbali zitafanywa na jumuiya ya maridhiano mkoa wa mbeya kupitia halmashauri zote ikiwa ni sambamba na kushiriki ligi ya samia amani cup.
Nae mwenyekiti wa maridhiano na amani mkoa wa Mbeya askofu Oscar Ongele amesema lengo la maadhimisho hayo nikudumisha Amani,mshikamano na upendo.
Akizungumza kwa niaba ya bank ya CRDB Meneja Wa Bank Hiyo Tawi La Mbeya Jeremia Msemo amesema wao kama benki wametoa miti zaid ya 2000 kufanikisha zoezi la upandaji miti litakalotekelezwa na jumuiya ya maridhiano mkoa wa mbeya.
Kwa upande wake balozi wa mazingira mkoa wa mbeya Chief Roketi Mwashinga amewata wananchi kulinda miti kwani imekuwa ikisaidia kuhifadhi vyanzo vya maji.
Baadhi ya wajumbe katika kamati ya maridhiano mkoa wa Mbeya wamewataka wananchi kuunga mkono jitihada hizo katika maeneo ambayo watafika kufanya shughuli za kijamii.
Katika uzinduzi wa wa maadhimisho ya maridhiano nchini mkuu wa mkoa wa mbeya ameongoza upandaji miti katika ofisi yake na kauli mbiu kuelekea katika kilele hicho inasema kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa,maridhiano na amani ndiyo nguzo yetu.