Wazazi washauriwa kuwapatia watoto lishe bora kupunguza udumavu nchini
6 February 2024, 18:11
Diwani wa kata ya Nanyala George Msyani wakati akiongea na wananchi wa kata hiyo(picha na Rukia Chasanika)
udumavu kwa watoto unasababishwa na baadhi ya wazazi na walezi kutowapatia lishe bora watoto wao pamoja na kutozingatia makundi ya vyakula.
Na Rukia Chasanika
Diwani wa kata ya Nanyala George Msyani amewataka wazazi na walezi kuzingatia utoaji wa lishe bora kwa watoto wao ili kupunguza udumavu nchini.
Diwani Msyani ametoa kauli hiyo katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 47 tangu kuzaliwa kwa chama cha mapindunzi yaliyofanyika katika kata ya Nanyala wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Nanyala Tagili Mwashalawe amesema watoto waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza wanatakiwa kwenda shule kwani zimejengwa kwa ajili yao.
Aidha akisoma taarifa ya utekelezaji katika maadhimisho hayo afisa mtendaji wa kijiji cha Nanyala Fariji Chonde amesema changamoto waliyonayo ndani ya chama cha mapinduzi ni upatikanaji wa kadi za kisasa za uanachama ambazo kwa muda mrefu hawajapata.
Akijibu taarifa hiyo mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu vifaa na takwimu wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Said Ngondo amesema kadi ziko tayari wilayani bado tu kuanza kuzisambaza katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo.