Waharibifu wa vyanzo vya maji, misitu Mbeya kuchukuliwa hatua
6 February 2024, 10:38
Na mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Beno Malisa Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenye siku ya upandaji miti Mkoani Mbeya ametoa mamlaka husika kuwachukulia hatua viongozi na wote watakaojihusisha na uharibifu wa Misitu na vyanzo vya maji Mkoani Mbeya.
Ameyaeleza hayo mara baada ya kuhitimisha Zoezi la upandaji wa Miti katika eneo la shule katika Kijiji cha Iwala Halmashauri ya Wilaya Mbeya.
Akitoa agizo hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mh Malisa ameendelea kuwasisitiza Wakurugenzi na Madiwani Mkoani Mbeya Kwenda kusimamia Sheria zilizopo za uhifadhi wa Misitu na Mazingira ili kukomesha vitendo vya uvamizi katika Maeneo hayo tengefu.
Kwa Mkoa wa Mbeya umeweka malengo kwa kila Halmashauri Mkoani humo kupanda miti Milioni 1.5 na kuisimamia ili kufanya tathmini ya miti iliyopandwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya Ndugu Stephen E Katemba amesema kuwa Halmashauri itaendelea kupanda zaidi Miti hii itasaidia kutunz Mazingira na kuingiza kipato kinachotokana na Miti hiyo ambapo takribani Milioni 420 imekusanya kutokana na Mazao yatokanayo na Miti hii ni kwa kushirikiana na Tfs
Kwa Upande wake Meneja wa Tfs Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Cosmas Ndakidemi Amesema kwa Mwaka huu Miti itatolewa hivyo wito kwa Wananchi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Kujitokeza kuchukua Miche na Kupanda kwa kipindi hiki cha Mvua.