Watalaam wa afya wasisitiza uwepo wa choo bora kwa kila kaya
1 February 2024, 17:47
Na Hobokela Lwinga
Timu ya watalamu wa afya imefanya ziara katika taasisi mbalimbali ikiwemo maeneo ya kutolea huduma za jamii lengo likiwa ni kukagua usafi wa mazingira, Kukagua muda wa matumizi ya dawa na usalama mahali pa kazi.
Katika ziara hii pamoja na mambo mengine wameikumbusha jamii kuhakikisha kila kaya, taasisi au mahali pa kazi wanachimba choo pamoja na kukisafisha mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Pia wamesisitiza kuhakikisha kila mkazi anaepuka kutupa taka ovyo na kutiririsha maji machafu ili kujikinga na mlipuko wa magonjwa hasa kipindupindu.
Wakati huohuo wamewakumbusha wamiliki wa maduka ya dawa baridi pamoja na taasisi zinazotoa huduma ya kwanza ( Shule, Mabasi, petrol station, vyuo nk) kuhakikisha wanahakiki mara kwa mara mwisho wa matumizi ya dawa ili kuepukana na Wananchi kupewa dawa zisizo stahili.