Mch. Mbazzah astaafu, aagwa na Baraka fm radio
1 February 2024, 17:12
Na Hobokela Lwinga
Kituo cha redio Baraka kimemuaga mfanyakazi wake mchungaji Nehemia Mbaza baada ya kustaafu kukitumikia kituo hicho kwa muda wa miaka 13.
Hafla ya kumuuaga mchungaji huyo imefanyika katika ukumbi mdogo wa chuo cha ufundi moravian uliopo kadege jijini mbeya.
Akizungumza katika hafla hiyo meneja wa radio Baraka Charles Amlike amesema ni vyema kila mtu ajitathimini katika utendaji wake wa kazi kabla ya kustaafu kwake kwani kila mtu ni lazma astafu kulingana na miongozo katika taasisi anayofanya kazi.
Aidha amlike amemtaka mchungaji huyo kuendelea kukiombea kituo mahala popote anapokuwa.
kwa upande wake mchungaji Gama Simbowe ambaye ni maratibu wa vipindi vya neno la mungu ambaye pia amekuwa akifanya kipindi pamoja cha ijue biblia amesema mchungaji mbaza kwake ni mwalimu katika mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya kujibu maswali redioni.
Nae Mkuu Wa Vipindi Radio Baraka Radio Mpoki Japhet Amesema Mch Mbaza Alikuwa Na Mchango Mkubwa Katika Radio Kwani Ni Miongoni Mwa waanzilishi wa radio.
Baadhi Ya Wafanyakazi Waliofanya Kazi Na Mchungaji Mbaza Wamesema mchungaji mbaza alikuwa msaada mkubwa kwa kituo kutokana na utendaji kazi wake huku wakijivunia upendo alikuwa nao kwa kila mfanyakazi.
Hata hivyo mchungaji Nehemia Mbaza ameishukru taasisi ya radio Baraka kwa kuwa nae begakwabega kipindi chote alichofanya kazi kama mtangazaji.