Bilioni 30 kukamilisha miradi ya maendeleo halmashauri ya Momba
1 February 2024, 08:51
Na mwandishi wetu, Songwe
Katika ripoti yake iliyosheheni utekelezaji wa miradi mingi na yenye thamani kubwa, Mkurugenzi amebainisha kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Halmashauri ya Wilaya ya Momba imepokea fedha zaidi ya Bilioni 30 ambazo fedha hizo zinetekeleza miradi katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Barabara, Maji, Umeme, Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Viwanda, Utalii na Uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Katika mkutano huo ulioandaliwa na Kurugenzi ya Habari Maelezo kutoka Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali ilitoa fursa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Songwe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe, Dkt. Francis Michael kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Serikali kwa kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha Mkutano huo uliwahusisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ambao walipata wasaa wa kuuliza maswali ya papo kwa papo na kujibiwa na Mkuu wa Mkoa Mhe Dkt. Francis Michael.
Mbali na Wakurugenzi lakini pia mkutano huo ulihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya husika pamoja na Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi mbalimbali pamoja na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Songwe