Taasisi ya takwimu Tanzania NBS kuboresha mfumo wa takwimu mtandao
31 January 2024, 10:20
Na Hobokela Lwinga
Kamisaa wa zoezi la Sensa na makazi ya watu ya mwaka 2022 ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda amesema kuna mkakati wa kuboresha mfumo kwa ajili ya ukusanyaji wa takwimu kwa njia ya mtandao itakayosaidaia kutoa taarifa kwa wakati huo huo.
Makinda ameyasema hayo kwenye semina ya Uwasilishaji, Usambazaji na Uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa waandishi wa habari wa Mikoa ya Mbeya, Iringa na Songwe iliyofanyika katika ukimbi wa mkapa jijini mbeya.
Nae mtaalamu wa habari na mawasiliano kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)said Said Ameir amesema takwimu zinazofanywa zinatumiwa na serikali katika kuandaa sera, kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo.
Kwa upande wake mtakwimu ofisi ya taifa ya takwimu Hellen Siriwa amesama kupitia sensa iliyofanyika mwaka 2022 idadi ya watu katika mkoa wa mbeya imeongezeka ambapo idadi ya watu ni kwa sasa ni 2,343754 ambapo ambapo wanaume ni 1,123828 na wanawake ni 1,219929.