Wakulima wa chai Rungwe wavikataa vyama vya ushirika
18 January 2024, 15:33
Na Ezra Mwilwa
Wakulima wa zao la chai wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wameviomba vyama vya ushirika kuwalipa mapema malipo yao ili waweze kuendeleza kilimo hicho kwa ufanisi.
Mwenyekiti wa wakulima hao Ndg. Asajile Mwasampeta amesema wamekua wakipata changamoto ya malipo huku vyama hivyo vikiwa na makato makubwa kwa wakulima.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wamedai kuwa kupitia kilimo hicho wanaweza kutimiza mahitaji muhimu ya kifamilia ikiwemo kupeleka watoto shule huku wakivikata vyama vya ushirika kikiwemo AMCOS.
Hivi karibuni Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe ametoa maelekezo kwa wakulima wadogo, wakubwa na wanunuzi wote wa chai kuwa chai yote ya Tanzania haitaruhusiwa kuuzwa nje ya utaratibu wa mnada wa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa Zao la chai ni mojawapo ya mazao ya kimkakati hapa nchini na kwamba Serikali imedhamiria kuimarisha kilimo cha zao hilo ili liendelee kuwa na tija kwa wakulima, wenye viwanda na Taifa kwa ujumla.