Acheni usanii,fanyeni kazi ya Mungu
18 January 2024, 12:10
Na Hobokela Lwinga
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde, Geofrey Mwakihaba amewataka wachungaji kuacha usanii na kurejea kwenye misingi ambayo Mungu amewatuma.
Amesema hayo katika ibada ya kuwabariki wachungaji 17 wa Kanisa hilo na kuwaingizi kazini katika usharika wa Tukuyu halmashauri ya wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Amesema idadi hii ya wachungaji ndani ya kanisa ikawe chachu ya kuwatumikia waumini kwa kuzingatia nini Mungu kawatuma na si kuwa wasanii.
Pia amewataka kufundisha kwa usahihi neno la Mungu na kuwa faraja kwa waumini, kwa kuwa Mungu haangalii uzoefu bali wito waliotumwa.
Mchungaji Ibrahim Abel Mwaipaja wa Usharika wa Ngamanga Jimbo la Kusini, amewataka waumini kumuomba Mungu na kuwalea watoto kwenye njia ya wokovu yenye baraka ili kuwaepusha na vitendo viovu.
Mbaraka huo wa wachungaji katika kanisa hilo umejumuisha wachungaji 17 wanaume 10 na wanawake 7 huku hali ya idadi ya wachungaji wanawake 7 kubarikiwa inadaiwa kuwa ni ongezeko kubwa tofauti na miaka ya nyuma.