Baraka FM

Mahindi Rungwe yaanza kukauka

16 January 2024, 14:16

Na mwandishi wetu

Katika Ukanda wa juu na kati katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe baadhi ya mashamba mahindi yameanza kukauka.

Pamoja na kukauka bado mvua inaendelea kunyesha katika kata zote ikilenga kustawisha mazao mbalimbali.

Wakulima Mnakumbushwa kuvuna kwa wakati , na kuyahifadhi vizuri ili kuepukana na SUMU KUVU ambapo huchochewa na kushindwa kuhifadhi mazao vizuri.

Sumu kuvu (Fangasi) hujitokeza baada ya mahindi kuoza na hivyo kukosa sifa ya matumizi kwa binadamu na wanyama wengine.

Sumu kuvu hupelekea mtumiaji wa mazao haya yaliyoathirika kupata ugonjwa wa kansa hatimaye kifo.