Milioni 207 yajenga kivuko kuunganisha Ivuna,Mjomba na Songwe DC mkoani Songwe
11 January 2024, 12:38
Na mwandishi wetu, Songwe
Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe amesema kuwa kivuko cha waenda kwa miguu kinachounganisha kata ya Ivuna na Mkomba pamoja na Wilaya ya Songwe kimegharimu kiasi cha Shilingi milioni 207 kimeweza kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwani sasa wananchi wataweza kuvuka katika kipindi chote cha mwaka na ameeleza kuwa mpango wa Serikali katika Wilaya ya Momba ni kuhakikisha linajengwa daraja la kudumu litakalokuwa na uwezo wa kupitisha mizigo.
“Eneo hili lilikua ni changamoto kwa wananchi maana kuvuka upande wa pili ilikuwa vigumu hasa kipindi cha masika lakini sasa kivuko hiki kimekuwa mkombozi na tuna mpango wa kujenga daraja la kudumu litakalopitisha mizigo ili wananchi wa meneo haya waweze kusafirisha mazao yao, kuna mazao kama alizeti, ufuta, mtama na mazao mengine yanayotakiwa kutolewa mashambani na kupelekwa sokoni’’, amesema Mbunge Mhe Condester.
Naye Bi. Rebeka Sichalwe.., Mkazi wa Kijiji cha Ivuna ameishukuru Serikali kwa kuwajengea kivuko hiko kwani hapo awali wananchi walikuwa wanapata shida kuvuka kutokana na maji mengi kujaa hasa kipindi cha mvua na kusababisha akina mama wengi kujifungulia njiani na pia hata wanafunzi walishindwa kuvuka kwenda shuleni.
“Tunaishukuru Serikali kwa kutuletea kiteputepu wengi tuliumia sana mto ukijaa wiki mbili hadi tatu tulikuwa hatuvuki kwenda kufanya kazi, akina mama tukikuta mto umejaa kujifungua ilikuwa ni shida, pia hata wanafunzi walishindwa kufanya mitihani wengi walifeli kwasababu ya mto huu kujaa maji, tunaishukuru sana Serikali kwa kujenga kivuko hiki a