Mapato ya ndani yanavyowapa tabasamu wananchi Rungwe
11 January 2024, 12:22
Na mwandishi wetu, Songwe
Furaha ya wakazi wa kata ya Kinyala ipo Mbioni kukamilika baada ya Halmashauri kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya kwa kutumia mapato yake ya ndani kwa gharama ya zaidi ya shilingi million 201.
Jumla ya majengo mawili yanajengwa likiwemo la wagonjwa wa nje (OPD) pamoja na jengo la Mama na mtoto.
Kutokana na kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali Halmashauri imeendelea kuwajali watu wake kwa kuwajengea miundombinu ya kutolea huduma ya elimu , afya, barabara, Mikopo isiyo na riba na mengine mengi.
Baadhi ya miundombinu mingine ni ujenzi wa shule ya Mchepuo wa kingereza katika eneo na Ilenge na Ushirika ambazo zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.
Aidha vyumba vya madarasa na zahanati mbalimbali zimekamilishwa na hivyo kufanya wakazi wa wilaya ya Rungwe kuendelea kunufaika na jasho lao linalotokana na kodi mbalimbali wanazotoa.
Barabara Kuelekea shule ya msingi Mpakani kata ya Matwebe imekamilika kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri hatua iliyorahisha wakazi wa kijiji hiki kusafirisha mazao yao kutoka shambani kwa urahisi na mafanikio makubwa.