Madini yasababisha uhaba wa wanawake Chunya mkoani Mbeya
9 January 2024, 18:08
Na Hobokela Lwinga
Wakati Takwimu sehemu Nyingi za Tanzania na Nchi nyingi za Afrika zikionyesha Wanawake kuwa wengi kuliko Wanaume Hali ni tofauti kwa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ambapo imeripotiwa kuwa Wanawake ni Wachache kuliko Wanaume.
Sababu za Wanawake kuwa Wachache kuliko Wanaume amezieleza RC Homera mara baada ya kuulizwa na Wanafunzi Kutoka Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi (NDC) walipowasili Ofsini kwake kumsalimia kabla ya kuanza Ziara Yao ya Mafunzo kwa Vitendo.
Homera Amesema chanzo cha uhaba wa wanawake katika halmashauri hiyo ni shughuli ya uchimbaji wa madini unaofanywa na Wananchi wa jinsia zote.
Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa licha ya uhaba huo wa wanawake bado mahitaji kwa wanaume kuhitaji wanawake umekuwa mkubwa hali inayosababisha mwanamke aonekane ni dhahabu.