NDC Mbeya yapokea wanafunzi toka nchi nne
8 January 2024, 14:11
Na Hobokela Lwinga
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera leo Januari 08, 2024 amekutana na wanafunzi kutoka Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi NDC waliofika mkoani Mbeya kwa lengo la kuendeleza mafunzo yao kwa njia ya vitendo.
Ziara ya wanafunzi hao imeshirikisha wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali wanaopata mafunzo chuoni hapo ambapo mbali na Tanzania ni Misri, Kenya, Rwanda na Burundi.
Brigedia General Charles James Ndiege Mkufunzi mwandamizi Kutoka Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi NDC-TZ ambaye ndiye Kiongozi wa Msafara huo Amesema dhumuni kubwa la Ziara ni kuwaimarisha Wanafunzi katika Masomo Yao ambapo wanajikita zaidi katika Mambo ya Kijamii,Kiuchumi Usalama na Ustawi.
Homera katika Kikao hicho akafanikiwa kuwaeleza Fursa za Kiuchumi na Kibiashara zilivyojaa Mkoani Mbeya.
“Sisi Mbeya tunaendelea kusonga Mbele tunazo fursa nyingi saana za Kiuchumi na Kibiashara Mfano Kwenye Madini tuko Mbali saana tunafukuzana na Geita tuu ila wengine hawatuwezi kabisa”
Kwa Habari ya Usalama wa Mkoa wa Mbeya Cde: Homera amewahakikishia Wanafunzi hao kuwa Mbeya ni Salama Wananchi wanaendelea kuchapa Kazi kwa Bidii Kila Mtu kwenye Nafasi yake.