Wananchi Rungwe waendelea kufurahia huduma za afya
30 December 2023, 09:04
Na mwandishi wetu
Huduma ya matibabu katika kituo cha afya Iponjola zimeanza leo rasmi tarehe 29.12.2023 ikiwa ni hatua ya kuwasogezea wananchi huduma hii muhimu karibu na makazi yao.
Kituo hiki kilichojengwa na Serikali kwa Kushirikiana na Wananchi kimegharimu zaidi ya shilingi million 500 .
Kituo cha a fya Iponjola kinapatikana katika kijiji cha Ngana mita chache kutoka katika shule ya msingi Ilalabwe.
Mpaka sasa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ina jumla ya Vituo vya afya 08 ambavyo ni Mpuguso, Kalebela, Masukulu, Ikuti, Kyimo, Ndanto, Isongole na Iponjola
Vituo vinavyoendelea na ujenzi ni pamoja na Kiwira, Masoko, Swaya, Kinyala na Malindo.
Aidha Wilaya ya Rungwe ina Hospitali ya wilaya Tukuyu ambayo hupokea rufaa zote kutoka katika vituo hivi vya afya na sehemu kutoka katika zahanati mbalimbali.
Kwa kuitikia hili Serikali imefanya upanuzi wa Hospitali ya wilaya kwa kujenga jengo na mama na mtoto kwa gharama ya zaidi ya shilingi million 700, Jengo la wagonjwa wa Dharura (EMD) , na Ujenzi wa jengo la ghorofa litakalotoa huduma ya Wagonjwa wa nje (OPD),Ofisi na Wodi za wagonjwa (Kwa gharama ya shilingi Billion 02.