Dkt.Tulia alivyombananisha afisa mipango miji mbeya kisa eneo la kanisa
30 December 2023, 08:52
Na Hobokela Lwinga
Mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 15 kati ya kanisa la Gofan, Jiji la Mbeya na kata ya Isanga, umechukua sura mpya baadaya Afisa mipango miji wa Jiji la Mbeya kukosa majibu ya namna walivyotwaa eneo hilo na kuongeza kwenye eneo la shule ya msingi Isanga kwa kuhamisha mipaka iliyowekwa mwaka 2017 na kuweka upya mwaka 2021.
Hayo yamejiri ikiwa ni siku chache baada ya kituo hiki kutangaza taarifa ya waumini wa kanisa Hilo kuiomba serikali kusaidia kutatua mgogoro wao, hali iliyo mvuta Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson kufika eneo hilo na kutaka kujua ilikuwaje Jiji la Mbeya walitoa mipaka ya awali na kuweka upya.
Baada ya kumsikiliza mchungaji wa kanisa la Gofan Mch. John Kimwaga, akatoa maelekezo kwa pande zote zinazo husika katika mgogoro huo kufika na nyaraka Ili zihakikiwe na haki itendeke juu ya eneo hilo linalogombaniwa.