Mbeya ya tatu uzalishaji wa chakula,wananchi washauriwa kuzalisha kwa tija
19 December 2023, 19:39
Na mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde Juma Zuberi Homera ameshiriki Mkutano wa Wadau Nyanda za Juu Kusini lililoandaliwa na Baraza la Kumshauri Rais kuhusu masuala ya Chakula na Kilimo chini ya Waziri Mkuu Mstaafu Mh: Mizengo Kayanza Pinda(Mtoto wa Mkulima) M/kit wa Baraza hilo ambao umefanyika katika Ukumbi wa Tughimbe Jijini Mbeya.
RC Homera katika hotuba yake ameueleza Umati wa Mkutano kuwa Mkoa wa Mbeya unazidi kupiga hatua katika Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Biashara Licha ya Kushika Nafasi ya Tatu lakini bado unazidi kupambana kuhakikisha unaidondosha Mikoa hiyo miwili iliyoitangulia.
Aidha Homera amewaalika Wananchi wote wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutumia Parachichi zinazozalishwa Mkoani Mbeya kwa kuwa ndio Mkoa pekee Nyanda za Juu Kusini unaozalisha Parachichi kwa Wingi.
Akifungua Kongamano hilo Mh: Mizengo Pinda Waziri Mkuu Mstaafu na M/kit wa Baraza amesema Serikali imeweka Mikakati Mathubuti wa Kuthubuti Upotevu wa Mazao utakaoambata na Uanzishwaji wa Mitambo ya Kuchakata Mazao Mbali mbali.
Kama tutaweza Kuthibiti Upotevu wa Mazao basi tutaanza kutanua Njia za Kuongeza Uzalishaji wa Mazao ya Biashara na kuyasafirisha Njee.
Halima Dendego Mkuu wa Mkoa wa Iringa akatoa Ushauri kwa Watanzania(Wakulima) “Ndugu zangu Wakulima Hatulimi ili tuisaidie Serikali tuache Kulalamika twendeni Shambani tukalime” Amesema Halima
“Lakini pia Mh: M/kit Wakulima wetu wanajitahidi kulima kwa Mstari na kuweka Mbolea Lakini swala la Mbegu bado ni Changamoto Wakulima wanatumia Mbegu ambazo sio Bora na hazina Uhakika Hivyo niwaombe jitihada ziongezwe katika kuzalisha Mbegu nyingi zaidi” Ameongeza Mh: Dendego