Mkuu wa mkoa wa Songwe akutana na uongozi wa kampuni za uchimbaji madini za rare earth matel na shanta
9 December 2023, 08:05
Na Mwandishi wetu,Songwe
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Dkt. Francis K. Michael, amekutana na Viongozi wa makampuni ya uchimbaji madini, RARE HEALTH METAL na SHANTA GOLD, katika ofisi yake , Wamefika kwa lengo la kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya miradi yao, changamoto wanazokutana nazo katika uchimbaji madini, na juhudi zao za kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kutoa mchango kwa jamii.
Maendeleo ya Mradi Wametoa ripoti ya maendeleo ya miradi yao na jinsi inavyochangia ukuaji wa sekta ya uchimbaji madini katika eneo la Songwe. Walisisitiza juu ya mikakati yao ya kuboresha ufanisi na kuendeleza teknolojia mpya ili kuhakikisha utendaji wa hali ya juu.
Viongozi hao wameeleza changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwa ni pamoja na masuala ya kijiografia, mazingira, na changamoto za Kupanda kwa Bei katika Soko la dhahabu. Pia, wamelezea juhudi zao za kukabiliana na changamoto hizo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Walisisitiza utayari wao wa kuendelea kushirikiana na mamlaka za serikali katika masuala ya kodi.
Aidha, wameelezea juhudi zao za kutekeleza takwa la kisheria la kurejesha faida kwa jamii (Corporate Social Responsibility). Walitaja miradi na programu wanazotekeleza katika wilaya ya Songwe, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu, elimu, na huduma za afya.
Mhe. Dkt. Francis, Amehimiza ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi kwa lengo la kuleta maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi.