Rungwe kupokea vitambulisho vya taifa 69,638
5 December 2023, 14:58
Na mwandishi wetu
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu amezindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya taifa (NIDA) leo tarehe 5.12.2023.
Zoezi limezinduliwa katika kata ya Kyimo tarafa ya Ukukwe.
Mhe Haniu ameeleza kuwa jumla ya vitambulisho 69638 vitatolewa kwa Wakazi wa wilaya ya Rungwe huku Kata ya Kyimo ikipokea jumla ya vitambulisho 2850.
Mhe Haniu amepongeza kwa hatua hii serikali imefanya na kuwa itarahisha utambulisho kwa wananchi katika kupata huduma mbalimbali.
Ameeleza kuwa uwepo wa kitambulisho kwa kila mkazi utasaidia kupata huduma mbalimbali hususani Mbolea ,Kibenki, Vitambulisho vya bima ya afya na hivyo kila mmoja hana budi kuvitunza kwani serikali imetumia gharama kubwa kuvitengene
Aidha Haniu amekemea vitendo vya kukaribisha wageni kutoka katika mataifa ya jirani bila kufuata taratibu na kuwa kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa watu na mali zao
Pamoja na hayo ameagiza watendaji wote wanaofanikisha upatikanaji wa vitambulisho kutoandikisha watu kutoka mataifa ya jirani.
Wakati huo huo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mhe Mpokigwa Mwankuga amepongeza Serikali kwa kazi hiyo nzuri hatua itakayosaidia upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi hasa katika msimu huu wa kilimo.