Askofu ashindwa kuchaguliwa kisa theluthi
17 November 2023, 21:30
Na Hobokela Lwinga
Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kaskazini (Arusha)limefanikiwa kufanya mkutano mkuu wa kanisa “Sinodi”iliyokuwa na jukumu la kupata viongozi wapya ikiwemo nafasi ya askofu katika Jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo nafasi ya askofu imeshindikana kumpata askofu kutokana na Wajumbe waliokuwa wanapigiwa kura walishindwa kufikia theluthi kwa mjibu wa katiba, hivyo nafasi hiyo imeachwa wazi mpaka bodi itakapotangaza tena.
Nafasi zingine ambazo zimepigiwa kura na mkutano mkuu ni nafasi ya mwenyekiti wa Jimbo ambapo mkutano huo umemchangua mch.Isaac Siame kuwa mwenyekiti,mch.Erick Mponzi kuwa Makamu wa mwenyekiti na mch.Jeremia Kibona kuwa katibu mkuu wa Jimbo.
Aidha katika Hatua nyingine mkutano huo umewachagua wenyeviti wa wilaya tatu katika Jimbo hilo ambapo waliochaguliwa ni mch.Merio,mch.Esther Mwasyoge na mch.Yohana Parkpuny wenyeviti hawa watapangiwa wilaya za kutumika na halmashauri kuu ya jimbo kwa mjibu wa katiba.