Coplo Kinyaga:Mnaweza kuisaidia jamii kuwa salama na majanga
17 November 2023, 21:21
Na Sifael kyonjola
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mbeya limetoa mafunzo kwa waandishi wa habari jinsi ya kukabiliana na majanga ya moto yanapotokea katika jamii inayowazunguka.
Mafunzo hayo yametolewa na afisa habari zimamoto na uokoaji mkoa wa Mbeya Koplo Ester Kinyaga katika ofisi za chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya.
Kinyaga amesema mafunzo hayo yametolewa kwa lengo la kuwapatia mafunzo waandishi wa habari juu ya elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga majanga mbali mbali yanapotokea katika shughuli zao.
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya Nebati Msokwa amesema kupitia mafunzo hayo waaandishi wa habari wamejifunza kuwa uokozi ni pamoja na kusaidia wajawazito waliokosa msaada,watu waliokumbwa na mafuriko pamoja na ajali ya moto.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Emanuel Lengwa na mwanaisha makumbuli wamesema mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na uokoaji wa wanyama wanapopata shida ya kutumbukia kwenye mito na mashimo ambapo mwananchi anatakiwa kutumia bure namba ya simu 114 kutoa taarifa mapema kwa kikosi cha jeshi la zimamoto na uokoaji ili apate msaada.