Zaidi ya wakulima 1326 na maafisa ugani 20 wamepatiwa elimu kilimo bora
15 November 2023, 17:51
Na Ivillah Mgala
Zaidi ya wakulima 1326 na maafisa ugani 20 kupatiwa elimu na mafunzo ya kilimo katika halmashauri ya wilaya ya mbarali mkoani Mbeya.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya mbarali mkoani Mbeya Kanali Denis Mwila katika hafla ya utiaji saini makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya watu wa marekani USAID ya kuwasaidia wakulima wa mbogamboga na matunda iliyofanyika katika kijiji cha mapunga kata ya igurusi.
Mkuu huyo wa wilaya amesema pamoja na hayo pia yapo mashamba darasa 21 yameanzishwa lengo likiwa ni kuwafundisha Kwa vitendo wakulima Ili waweze kulima Kwa tija.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Mradi wa USAID Kilimo Tija Antonio Coello amesema zaidi ya bilioni nne zimekopeshwa Kwa wakulima wa mboga mboga na matunda katika halmashauri 19 nchini zinazofanya kazi na mradi huo unaofadhiliwa na USAID.
Naye mkulima wa mfano wilaya ya mbarali Fanuel Vahaye amesema wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi kuliko faida ikiwemo ukosefu wa soko,ucheleweshwaji wa pembejeo pamoja kutokuaminiwa na taasisi za kifedha.