Maelfu Mbeya Wajitokeza Kupima Afya Kwenye Maadhimisho Ya Siku Ya Kisukari Duniani
14 November 2023, 20:41
Na Daniel Simelta
Tarehe 14 Novemba kila mwaka, duniani kote huadhimishwa Siku ya Kisukari Duniani. Maadhimisho haya yanafanyika kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu kisukari, kuhamasisha watu kuchukua hatua za kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo, na kushirikiana katika kupambana na changamoto zinazowakabili watu wanaoishi na kisukari.
Katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani yalikuwa ya kipekee na yenye tija ambapo hospitali kupitia timu ya wataalamu wa afya imetoa elimu na ushauri kuhusu kisukari, chunguzi wa afya bila malipo pamoja na uchangiaji damu salama kwa jamii.
Akiongea wakati wa zoezi hilo Dkt. Alumbwage Nyagawa mratibu wa zoezi hilo amesema lengo kubwa ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuhakikisha wananchi wanapata nafasi ya kupima afya zao pamoja na kupatiwa elimu, uchangiaji damu sambamba na huduma za upimaji wa magonjwa mbalimbalimbali yasiyo ambukiza.
“..sisi kama hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya tumekuja kusogeza huduma kwa wananchi ili kuwawezesha kupima afya, kutoa elimu, pamoja na wao kuweza kuchangia damu.” – Dkt.Alumbwage Nyagawa
Aidha. Dkt. Alumbwage Nyagawa ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwa kuwa wengi hufikiri wana afya njema wawapo majumbani
Jambo ambalo si kweli kwani wengi wao baada ya vipimo mahali hapa wamekutwa na changamoto mbambali.
“..kwasababu watu wengi wanakaa majumbani wanajiona wapo sawa lakini kwa uhalisia wanakuwa na changamoto za kiafya.” – Dkt.Alumbwage Nyagawa
Epafra Isaya ni mwananchi mwenye uziwi aliyejitokeza kapata huduma ya upimaji wa afya amesema amefurahishwa na huduma nzuri alizopata mahali hapo kwa kuwa amepata nafasi ya kupima shinikizo la damu, ugonjwa wa kisukari, hivyo amefurahishwa na huduma hizo kwa kuwa wao viziwi wamekuwa wakipata wakati mgumu sana kupata elimu juu ya magonjwa yasiyoambukiza.
“..nimefurahi kwasababu sisi viziwi mara nyingi hatuna uelewa wa magonjwa haya yasiyoambukiza.