Dkt.Tulia azindua ofisi na kugawa bodaboda Kawetele jijini Mbeya
14 November 2023, 20:35
Na Hobokela Lwinga
Spika wa Mabunge Duniani ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson amezindua tawi la Bodaboda Kawetele Jijini Mbeya pia kukabidhi mkopo wa pikipiki wenye thamani ya shilingi milioni kumi na tano na kuchangia shilingi milioni mbili kuimarifa mfuko wao.
Dkt Tulia Ackson amesema lengo la taasisi yake ni kuwakwamua wananchi kiuchumi.
Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji la Mbeya Aliko Fywanda amesema Bodaboda ni sehemu ya ajira hivyo watapambana na watu wataojaribu kuanzisha vurugu.
Madiwani wa Kata za Mwasenkwa na Itagano wamepata fursa ya kutoa neno ambapo wamesema jitihadi za Dr.tulia ni kuwatumikia wananchi wote.
Hafla hiyo imehudhuriwa na vikundi mbalimbali kwa lengo la kumpongeza kuchaguliwa kuwa Rais wa Mabunge Duniani(IPU) wakiwemo viongozi wa Daladala na Wauzaji wa vyuma chakavu.
Hii ni ziara yake ya kwanza Jimboni kwake tangu arejee nchini baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Mabunge Duniani uchaguzi uliofanyika Angola oktoba 27,2023.