Dr.Tulia:Toeni elimu huo ndio wajibu wenu kama ustawi wa jamii
14 November 2023, 19:45
Na Deus Mellah
Spika wa bunge la jamhuri wa muungano wa tanzania ambaye pia ni mbunge wa jimbo la mbeya mjini Dr Tulia Akson amewataka mafiasa ustawi wa jamii nchini kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu jamii hasa katika kuhakikisha jamii inakuwa na usawa.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamono la kitaaluma pamoja na mkutano wa mwaka wa wanataaluma ya ustawi wa jamii Tanzania TASWO linaloendelea katika ukumbi wa tugimbe jijini mbeya.
Dr tulia amesema maafisa wanawajibu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kwani bado elimu inahitajika juu ya uelewa wa mambo na kufanya tafiti mbalimbali .
Naye Salma Fundi ambaye ni makamu mwenyekiti wa TASWO amesema wao kama wanaustawi wa jamii watahakikisha wanaenda kuyafanyia kazi yale yote ambayo wameagizwa na spika.
kwa upande wake afisa tawala wa mkoa wa mbeya Mohamed Fakili amewataka maafisa ustawi wa jamii nchini kufanya kazi kwa weledi ili wawe mfano wa kuigwa katika jamii.
Songoro Jumbe Msongo katibu mwenezi wa wataaluma wa ustawi wa jamii Tanzania amesema kuwa wataenda kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili jamii iwe yenye usawa.