34 mbaroni kwa uharifu Mbeya
13 November 2023, 18:57
Na Hobokela Lwinga
Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya limewakamata watuhumiwa 34 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo utoroshaji madini, uhamiaji haramu, uvunjaji na wasambazaji wa noti bandia.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kutorosha madini ni Edward Kessy na Feisal Abdullah wakazi wa Makongolosi wakiwa na dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 141.
Aidha jeshi hilo linawashikilia watu wawili James Mwamatepela Na Wille Mwandwani wakazi wa kijiji cha ngyeke wilaya ya kyela kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia 42 za shilingi 10,000.
Katika tukio lingine jeshi hilo linawashikilia wahamiaji haramu 16 raia wa ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Kamanda kuzaga amesema huko wilaya ya rungwe jeshi la polisi limewakamata watuhumiwa watatu wakiwa na vifaa vya kuvunjia majengo kwa lengo la kufanya uhalifu.
Hata hivyo kamanda wa polisi mbeya Benjamini Kuzaga amesema kuwa watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.