Wanavyuo washauriwa kujiajiri na kuondokana na makundi maovu
7 November 2023, 12:25
Vijana wa rika mbalimbali wanaomaliza masomo yao kwenye vyuo tofauti nchini wametakiwa kutojiingiza katika makundi yasiyofaa kwani yanaweza kukatisha ndoto zao za baadaye.
Na Deus Mellah
Wito huo umetolewa na msimamizi wa miradi kanisa la Moravian jimbo la Kusini Magharibi Esau Swila wakati akizungumza katika mahafali ya wanafunzi wa kikristo yaani University Student Christian Fellowship USCF katika Chuo cha Ufundi Moravian jijini Mbeya.
Amesema vijana wengi wakimaliza vyuo mbalimbali wakirudi nyumbani kwao wakati wanasubiri ajira huwa wanajiingiza katika makundi yasiyofaa kama vile uvutaji wa bangi kucheza kamali na kujihusisha kwenye mahusiano hali inayosababisha kutotimiza malengo yao.
Kwa upande wake mratibu wa vyuo vikuu na kati vilivyopo mkoa wa mbeya na songwe mch Whisper Siwiti amewataka vijana hao kufanya kazi za kujiajiri ili waweze kujiingizia kipato kwani wamepata uzoefu wa fani mbalimbali.
Naye rais wa chuo cha ufundi Moravian ambaye pia ni kiongozi wa USCF Crein Mlomba amesema kile walichofundishwa na walimu wao kuhusu masuala ya ufundi wataendelea kuyafanyia kazi maana ndo hazina yao ya baadae.
Nao baadhi ya wanafunzi wa chuo cha ufundi Moravian wamesema kuwa wakieenda mtaani watahakikisha wanafanya shughuri mbalimbali zinazoweza kuwaingizia kipato na kuachana na kujiingiza katika makundi yasiyofaa.