Polisi Mbeya yakanusha kukamatwa kwa wakili Mwabukusi na Mdude Nyagali
4 November 2023, 00:14
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo rasmi kuwa Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali wamekamatwa na Polisi wakiwa na baadhi ya waandishi wa habari.
Na Hobokela Lwinga
Taarifa hizo ni za upotoshaji, hazina ukweli wowote, ni kwamba leo Novemba 03, 2023 majira ya asubuhi Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali waliitwa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya kwa ajili kukabidhiwa barua yenye majibu ya ombi lao la kufanya maandamano ya amani na mkutano waliyopeleka kituo kikuu cha Polisi siku ya tarehe 02 Novemba, 2023.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo rasmi kuwa Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali wamekamatwa na Polisi wakiwa na baadhi ya waandishi wa habari.
Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewana na kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamini Kuzaga inasema kuwa Taarifa hizo ni za upotoshaji, hazina ukweli wowote, ni kwamba leo Novemba 03, 2023 majira ya asubuhi Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali waliitwa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya kwa ajili kukabidhiwa barua yenye majibu ya ombi lao la kufanya maandamano ya amani na mkutano waliyopeleka kituo kikuu cha Polisi siku ya tarehe 02 Novemba, 2023.
Hivyo kutokana na kutojulikana anuani zao na baada ya wahusika kuonekana eneo la jirani na ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ndipo wahusika waliitwa ofisini hapo na kisha kukabidhiwa barua yenye majibu ya ombi lao kupitia Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa umma kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo, ni vyema kusubiri kupata taarifa kupitia vyanzo sahihi.