Hatimaye Moravian jimbo la Kusini Magharibi lapata askofu
2 November 2023, 16:11
Miongoni mwa matukio ambayo yalikuwa yakisubiriwa kwa waumini wa kanisa la Moravian ni hili la uchaguzi wa askofu ambaye alikuwa anasubiriwa kuchukua nafasi iliyoachwa baada ya askofu Alinikisa Cheyo kustaafu.
Na Hobokela Lwinga
Mkutano mkuu wa sinodi ya dharula ya uchaguzi wa askofu umemchangua mchungaji Robart Pangani kuwa askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo wa askofu, askofu kiongozi wa kanisa la Moravian Tanzania KMT Conrad Sikombe Nguvumali amesema mchungaji pangani amepata kura 317 zaid ya theluthi 296 dhidi ya mchungaji mwambalaswa aliyepata kura125.
Askofu Nguvumali amesema kutokana na sinodi hiyo kuwa ya dharula kwa ajili ya askofu hivyo mchungaji pangani ataendelea kuwa mwenyekiti mpaka sinodi ijayo kwa mjibu wa katiba ya Kanisa.
Kwa upande wake askofu Yona Ezekiel wa jimbo la tabora amesema huu ni mpango Mungu kwa Kanisa kupata askofu mchungaji Robert pangani.
Hata hivyo wakizungumza kwa niaba ya kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi,katibu mkuu ndugu Israel Mwakilasa na Makamu mwenyekiti wa jimbo mch.Asulumenye Mwahalende amewashukru wote waliofanikisha mkutano huo.
Baada ya kuchaguliwa kuwa askofu mchungaji Robert Pangani amesema anamshukru Mungu kupitia Wajumbe wa mkutano mkuu wakanisa kumpa nafasi ya kuliongoza kanisa ameomba ushirikiano.
Uchaguzi huo wa askofu umefanyika kufuatiwa mtangulizi wake askofu alinikisa cheyo kustaaafu.