Vyoo vyatajwa kuwa sababu ya chanzo cha polio
31 October 2023, 15:37
Mgonjwa mmoja wa polio kwa mjibu wa wataalumu wa afya anapobainika kupata maambukizi anatajwa kuweza kuambukiza watu Zaidi ya 200 kwa wakati mmoja.
Na Hobokela Lwinga
Serikali inatarajia kutoa chanjo ya awamu ya pili ya polio katika mikoa sita ya nyanda za juu kusini kwa watoto wote wenye umri wa miaka chini ya nane.
Akizungumza na kituo hiki kupitia kipindi cha nuru ya asubuhi afisa chanjo kutoka makao makuu ya wizara ya afya Dodoma penford Joel amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanazingatia zoezi ambalo linatarajiwa kufanyika November 2 hadi 5 mwaka huu.
Bw.penford amesema serikali imeendelea kununua chanjo hizo kwa gharama kubwa lengo ni kuwalinda na kuwakinga wananchi wake na ugonjwa huo.
Aidha amesema zipo athari nyingi ambazo zinajitokeza pindi mtu anapopata ugonjwa wa polio ikiwemo ulemavu wa kudumu wa viungo .
Amesema ugonjwa wa polio unasababishwa na kuenezwa na uchafu hasa matumizi ya vyoo usio sahihi.