Songwe madereva wapigwa stop ulevi
30 October 2023, 17:35
Miongoni mwa sababu kubwa ya ajali za barabarani ni kwa baadhi ya madereva kutumia vilevi kupindukia wanapokuwa barabarani wakiendesha vyombo vya vya moto,baada ya kuini hili kumekuwepo na ukaguzi uanao fanywa na jeshi la polisi kwenye vituo vya kuazia safari
Na Josea Sinkala.
Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani Wilaya ya Songwe limesema ulevi ni moja kati ya sababu zinazochochea ajali za mara kwa mara zinazozuilika hivyo kuwataka madereva hususani wa pikipiki kuacha kuendekeza ulevi.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Polisi wa usalama barabarani Wilaya ya Songwe (DTO) Mkaguzi msaidizi wa Polisi Charles Mosabi Wambura wakati akizungumza na mamia ya madereva wa vyombo vya usafirishaji kutoka kata za Mkwajuni na Saza Wilayani Songwe.
Wambura amesema ulevi na mwendo kasi bila kuchukua tahadhari ni baadhinya sababu zinayowafanya madereva kujiamini kupita kawaida wakiwa barabarani hivyo kuchochea kushamiri kwa ajali za mara kwa mara.
“Sasa hivi kwenye Wilaya yetu (Songwe) kumekuwa na ajali mfano ajali iliyotokea juzi kisa tu bodaboda alikuwa mwendokasi na wengine ulevi. Ndugu zangu msiendeshe vyombo vya moto mkiwa mmelewa, bora ukiona umelewa chukua bodaboda mwingine akupeleke nyumbani, Songwe bila ajali inawezekana”, Amesema DTO Charles Wambura.
Hata hivyo mkuu huyo wa Polisi wa barabarani Songwe ametoa ole kwa madereva watakaoendelea kukiuka kwa makusudi sheria za usalama barabarani.
“Bodaboda na watumiaji wote wa vyombo vya moto sheria inasema ukifika Zebra hata kama hakuna mtu anayevuka inakubidi usimame au upunguze kabisa mwendo ndipo upite hapo itasaidia hata sisi wenyewe kuwa salama. Nawaomba tuzingatie sheria zote za barabarani na uvaaji wa kofia ngumu. Mimi ilishawahinitokea ajali nikiwa kwenye pikipiki nisingekuwa na kofia yangekuwa mengine”, amesisitiza Mkuu huyo wa Polisi wa Usalama barabarani Wilayani Songwe.
Katika kikao hicho mgeni rasmi alikuwa ni mkuu a Wilaya ya Songwe Mhe. Solomoni Itunda aliyesisitiza umuhimu wa madereva wote wanaotoa huduma za usafiri na usafirishaji kuzingatia sheria na kufanya kazi kwa malengo ili kutimiza ndoto zao.
Mkuu wa Wilaya amewaahidi madereva hao Serikali yake kuwaunga mkono kwa hali na mali katika mipango yao ikiwa wataungana kujenga Chama cha maafisa wa usafirishaji Wilaya ya Songwe ikiwemo kuwapatia shamba kubwa kwa ajili ya kujiwekeza kwenye kilimo ili kujiinua kiuchumi.
Silas Edward ni Balozi Usalama Barabarani na dereva na Edson Chamkanga ambaye pia ni Dereva bodaboda wameishukuru Serikali ya Wilaya ya Songwe kwa kuunda umoja huo na kudhamiria kutoa shamba kwa ajili ya bodaboda kujikita pia kwenye kilimo ili kujiinua kiuchumi na kutimiza