Mzee miaka 80 ukutwa na Gobole bila kibali
26 October 2023, 18:28
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na oparesheni, misako na doria zenye tija kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.
Na Hobokela Lwinga
mzee wa miaka 80 mkazi wa Kijiji cha Madundasi Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya aitwaye Pascal Mwango anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kupatikana na bunduki aina ya Gobole bila kuwa na kibali cha umiliki halali.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa wa mbeya ACP Benjamini kuzaga amesema mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 20, 2023 huko Masenjele ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha.
Aidha Katika upekuzi alikutwa na bunduki moja [gobole], risasi [golori] 35, unga wa baruti ukiwa kwenye mfuko wa plastiki, kisu 01, kiberiti 01 na fataki mbili za kulipulia bila kibali cha umiliki halali wa vitu hivyo.
Hata hivyo amesema Mtuhumiwa amekuwa akifanya uhalifu kwa kuwinda na kuua Wanyama pori ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Jeshi la Polisi lipo katika kampeni ya msamaha wa usalimishaji silaha haramu kwa hiari iliyoanza Septemba mosi na inatarajiwa kumalizika Oktoba 31, 2023. Hivyo ametoa wito kwa wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha kwa hiari.