Waumini watakiwa kuachana na tabia za unafiki ndani ya dini zao
23 October 2023, 13:25
Mtu anapoamini ni ishara ya kufanya vitu vingi kwenye maisha ndivyo ilivyo pia mtu akiamini katika imani ya dini anapaswa kuishi maisha kulingana na imani ya dini yake, kwa wakristo wanaaswa kuishi maisha kama aliyoishi Yesu akiwa duniani.
Na Hobokela Lwinga
Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi limefanikiwa kufanya mkutano mkuu wa kwaya kuu katika ushirika wa Mlima Reli huku mkutano mwingine kama huo ukitarajiwa kufanyika mwakani 2024 katika kanisa la Moravian eneo la Misheni ya Iringa.
Katika hali hiyo makamu mwenyekiti na mlezi wa idara ya kwaya kuu jimbo la Kusini Magharibi Mch. Asulumenye Mwahalende amemuelekeza mwenyekiti wa misheni ya Iringa Mch. Bora Msola kuandaa mazingira mazuri ya kupokea ugeni huo ambao utakuwa na washiriki zaidi ya 400.
Mch. Mwahalende amewatakia viongozi wote kuanzia ngazi ya ushirika maandalizi mema ya mikutano kwa mwaka ujao .
Wakati akihubiri katika ibada hiyo mwenyekiti wa misheni ya iringa kaninsa la Moravian Mch. Bora Msola amewataka waumini kuacha tabia ya unafiki katika kufanya kazi ya Mungu.
Sambamba na hayo mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania wilaya ya mbalizi mch.Erica Samwanijembe amelishukru jimbo kwa kufanya mkutano huo wilayani kwake.
Hata hivyo katibu wa idara ya kwaya na uinjilisti jimbo la kusini magharibi mch.Peter mbugi Amewashukru washiriki wote wa mkutano kwa namna ambavyo wamejitoa katika kumtumikia mungu.
Kwa upande wake mshindi wa mziki katika mkutano huo Kisa Kayuni amelishukru kanisa kwa kutambua vipaji,na vipawa kwa waumini wake.