Wazazi na walezi msiwaachie walimu watoto wenu
19 October 2023, 18:39
Hivi karibu kumekuwa masuala ya kikatili ambayo yamekuwa Yakifanywa kwa wanafunzi na walimu wao,kitendo hicho kimekuwa kikwazo na kuondoa iman ya kuwaamini baadhi ya walimu.
Na Daniel Simelta
Wazazi na Walezi mkoani Songwe, wametakiwa kuimarisha malezi kwa watoto wao na sio kuwaachia walimu jukumu hilo.
Akizungumza wakati akitoa elimu ya Ushirikishwaji Jamii kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mtumbo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya, amesema endapo malezi ya watoto yataimarishwa na kusimamiwa vyema ni wazi kuwa hakutakuwa na mmomonyoko wa maadili utakaochangia watoto kutofikia malengo yao kielimu.
Sanjali na hayo Kamanda Mallya amesema ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto ni lazima kuimarisha malezi bora kwa watoto wetu ikiwa ni pamoja na kufuatilia mabadiliko ya tabia zao.
Kwa upande wa walimu wa shule hiyo mbali ya kupongeza jitihada mbalimbali za Jeshi la Polisi katika kuyafikia makundi yote kwenye jamii waliahidi kuwafikishia ujumbe huo wazazi wa wanafunzi kupitia vikao vya wazazi shuleni hapo.