Baraka FM

Kisa simu mwanaume ampiga mke wake mpaka kufa Mbeya

17 October 2023, 18:09

Huu ni mfano wa simu iliyosababisha kifo cha Faraja Mwaigaga(Picha na mtandao)

Wakati Mungu anamuumba mwanadamu yaani adamu aliona si vema akishi pekee yake akampatia msaidizi wake ambaye ni eva ili waishi pamoja tena kwa furaha,hali hiyo imegeuka karaha kwa wanandoa hawa kujikuta wakiingia kwenye mgogoro kisa simu na kusababisha kifo kwa mmoja wapo.

Na Hobokela Lwinga

Mwanamke mmoja aitwaye Faraja Mwaigaga amefariki dunia baada ya kupigwa na mume wake wakati wakigombea simu.

Tukio hilo limetokea kitongoji cha Estate kata ya bonde la Songwe wilaya ya Mbeya ambapo mwanamke huyo alipoteza maisha wakati akikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Picha ya marehemu faraja mwaigaga (kushoto) akiwa na mme wake Florence Mapema(kulia)

Baadhi ya mashuhuda wamesema walipata taarifa kutoka kwa mtoto wa marehemu na kudai kuwa mara kadhaa mwanaume huyo amekuwa akimpiga marehemu.

Sauti za mashuhuda wa tukio

Kwa upande wake kaimu Mwenyekiti wa kitongoji cha Estate Nilo Kapinga amekemea unyanyasaji wa aina hiyo sambamba na kueleza kuwa mtuhumiwa amekamatwa kwa hatua zaidi za kisheria.

Kaimu Mwenyekiti wa kitongoji cha Estate Nilo Kapinga(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya kaimu Mwenyekiti wa kitongoji cha Estate Nilo Kapinga

Hata hivyo kituo hiki kinaendelea kufanya jitihada za kumpata kamanda wa polisi Mbeya ili kupata ufafanuzi zaidi wa tukio hilo kwani  baada ya kufika ofisini kwake alikuwa kwenye majukumu mengine nje ya ofisi.