Wavenza: Saidieni watoto yatima waishi kama watoto wengine
17 October 2023, 17:30
Kwenye jamii kuna msemo unasema motto wa mwenzako ni wako ,hii inamaana kuwa kila mtoto anapaswa kupata mahitaji yote kama watoto wengine unapopata nafasi ikiwa ni pamoja na chakula,elimu na malazi.
Na Deus Mellah
Jamii nchini imetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia watoto wenye uhitaji wanaoishi katika mazingira magumu ili nao waweze kujikimu kimaisha.
Wito huo umetolewa na msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha Mbozi mission Annis Wavenza baada ya watoto wa shule ya Jumapili kutoka kanisa la Moraviani ushirika wa Saza Chunya kutembelea kituo hicho kilichopo eneo la mbozi mission mkoani wa Songwe.
Msimamizi huyo Wavenza amesema kituo hicho kwa sasa kina watoto tisa na wengine wapo shule mbalimbali wanasoma.
Naye mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi ushirika wa Saza Chunya Enerd Mwashibale amewashukuru wasimamizi wa kituo hicho kwani wamekuwa wakiwahudumia watoto mbalimbali bila kujali dini wala kabila.
Nao baadhi ya watoto wa shule ya jumapili pamoja na walimu wao wamesema wamewasaidia watoto hao mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni,Nishati umeme(solar) pamoja na nguo.