Wazazi washauriwa kutengeneza mazingira mazuri kuondoa utoro kwa wanafunzi
17 October 2023, 15:48
Mazingira mazuri kwa wanafunzi kunatajwa kuwa chanzo cha mafaniko kwa wananfunzi wengi, wanafunzi wengi wameshindwa kufanya vizuri kwenye masomo yao kwa sababu ya kukutana na changamoto kwenye mazingira ya shule na nyumbani.
Na Deus Mellah
Wazazi na walimu kwa kushirikiana kwa pamoja wanaweza kutatua tatizo la utoro wa wanafunzi katika shule ya sekondari Imezu iliyopo kata ya Inyala mkoani Mbeya.
Hayo yamesemwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Ferdinand Skuliet wakati akizungumza na kituo hiki kuhusu namna walivyoshirikiana na wazazi kutokomeza utoro katika shule hiyo.
Amewataka wanafunzi wanaojiandaa na mtihan wa taifa kuwa watulivu wakati wakisubiri mtihani huo.
Naye Elizabet Mbwete ambaye ni mwenyekiti wa bodi katika shule hiyo amewaasa wanafunzi hao kuendelea kujisomea ili kila mmoja aweze kufaulu.
Mmoja wa wanafunzi wanaoenda kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne amesema amejianda vizuri katika mtihani utakaoanza nov 13,mwaka huu.