Utoro chanzo ufaulu kushuka kwa wanafunzi kidato cha nne
3 October 2023, 17:17
Wazazi na walezi ni lazima wawe karibu na watoto wao ili kuhakikisha wanazingatia masomo yao na kufika shuleni kwa wakati ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.
Na Rukia chasanika
Imeelezwa kuwa utoro wa wanafunzi wa shule ya sekondari Shikula iliyopo kata ya Nanyala mkoani Songwe unasababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao.
Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Nanyala George Msyani wakati akizungumza katika mahafali ya 16 ya shule hiyo.
Msyani amesema ili kukomesha tabia hiyo ni lazima wazazi na walimu washirikiane kwa pamoja kukemea tabia hiyo.
Pia Msyani ameongeza kuwa ni wajibu wa jamii kuwa na mchango wa kuwasaidia wanafunzi hao ili kuwaongezea hali ya kuwa na bidii katika masomo .
Naye mkuu wa shule hiyo Emmanuel Kayombo amesema shule yao inakabiliwa na changamoto ya upungugu wa walimu wa sayansi na hisabati hivyo wanaiomba serikali iwasaidie.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa niaba ya wanafunzi Ronick Mwankota amesema wamefanikiwa kuendeleza miradi wa ufugaji mbalimbali katika shule hiyo.