Tulia traditional dances festival yafana Mbeya
29 September 2023, 10:46
Mziki ni sehemu ya maisha maisha ya binadamu,jamii inasisitizqwa kuenzi na kufuatilia mziki wa asili ili kudumisha mila,destri na tamaduni
Na Ezra Mwilwa
Mstahiki meya wa jiji wa Mbeya Dormohamed Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Mbeya kuyatumia maonesho ya ngoma za asili kupata fursa ili kujiinua kiuchumi.
Ameyasema hayo wakati akifungua maonyesho ya ngoma za asili mkoa wa Mbeya yaliyofunguliwa rasmi leo katika viwanja vya airpot ya zamani jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa maandalizi ya maonyesho hayo Adam Mwakatumbula amesema wanamshukuru dk. Tulia Akson kwa kuanzisha tamasha hilo ambalo linawaunganisha watu mbalimbali na kudumisha umoja wa kitaifa.
Aidha katibu wa machifu mkoa wa mbeya Ilanga Mwanamtwa amesema maonyesho hayo yatafanyika kwa amani hivyo watu wote wanakabishwa kushiriki.
Diwani wa kata ya Iyela Mussa Ismail amesema kufanyika kwa tamasha hilo katika kata yake kunasaidia kuinua uchumi wa kata yake.