WHO: Tuna imani na wanahabari katika kutatua changamoto za jamii
29 September 2023, 10:04
Jamii imekuwa na uelewa mdogo sana juu ya makundi ya ya watu wenye ulemavu ,hivyo basi katika kuondoa dhana ya unyanyapa wwa makundi yenye ulemavu serikali kupitia wadau imekuwa ikitoa elimu kuwezesha kuondokana na hali hiyo.
Na Hobokela Lwinga
Katika kuelekea kilele cha siku ya wiki ya viziwi dunia waandishi wa habari nchini wametakiwa kutumia kalamu zao kwa kuandika habari zinazoibua changamoto zinazolikabili kundi la watu wenye ulemavu.
Wito huo umetolewa na afisa jinsia kutoka shirika la afya Duniani WHO wakili Mary Kessi katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini ambayo imefanyika katika ukumbi wa mkapa uliopo mkoani Mbeya.
Wakili Mary amesema ili uweze kufanikisha jambo lolote kwenye jamii ni muhimu kutumia tasnia ya habari kwani inamchango mkubwa na inaaminika na jamii.
Nae Afisa mkuu ustawi wa jamii kutoka wizara ya afya Dibogo Raymond amesema wizara itahakikisha makundi yote yanafikiwa ikiwa ni pamoja na kupunguza changamoto zinazoyakabili makundi yenye ulemavu.
Kilele cha maadhimisho ya wiki ya viziwi kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Mbeya September 30 mwaka huu yakiwa na kauli mbiu isemayo” Ulimwengu ambao viziwi popote walipo wanaweza kutumia lugha ya alama”.