Mbeya yazindua huduma ya utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto
21 September 2023, 15:47
Mkoa wa Mbeya ni moja ya mkoa wa Nyanda za Juu Kusini ambao umeanza leo zoezi la utoaji wa chanjo kwa watoto wenye umri wa miaka nane hii ni kutokana na uwepo wa mkoa wa katavi kuwa na kisa cha mgonjwa mmoja wa ugonjwa huo.
Na Sadock Mwaigaga
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amewataka wananchi kuhakikisha wanawapatia watoto wao chanjo ya polio ili kuwakinga na ugonjwa wa polio.
Mkuu wa mkoa Homera amesema hayo wakati akizindua utoaji wa chanjo ya matone ya polio katika kata ya Iyela ambayo itafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia septemba, 21 hadi septemba 24 mwaka huu.
Homera amesema chanjo hiyo haina madhara kwa watoto na wamejipanga kufika kila eneo kutoa huduma hiyo.
Kwa upande wao madaktari waliohudhuria katika uzinduzi huo wamesema chanjo hiyo ni ya muhimu kwa kila mtoto kujikinga dhidi ya ugonjwa polio unaoweza kusababisha mtoto kupooza na watahakikisha kila mtoto anapata chanjo hiyo.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mbeya wameipongeza serikali kwa kutoa chanjo hiyo kwa watoto na wa namewaomba wahudumu wa afya kupita katika shule za watoto mbalimbali ili wapatiwe chanjo hiyo.