Mafunzo ya TADIO baraka fm yawapa shangwe wafanyakazi
20 September 2023, 16:40
Kwenye maisha ya binadamu kujifunza ni jambo jema na ukipata nafasi inakupa fursa ya kufanikiwa kwenye maisha,TADIO ni moja ya mtandao unaotoa fursa ya kumjenga mtu ili kutumia fursa zilizopo hasa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.
Na Hobokela Lwinga
Kituo cha radio Baraka cha jijini Mbeya kimeyapokea na kuyafurahia mafunzo kwa wafanyakazi wake yaliyotolewa na shirika la maendeleo ya habari Tanzania tadio.
Wakizungumza mara baada ya kupokea mafunzo hayo kutoka kwa mkufunzi kutoka tadio Amua Rushita baada ya kufika katika ofisi za radio hiyo wamesema mafunzo hayo ni mazuri kwani yanawajengea imani kwa watu wanaofanya nao kazi pindi wanapohitaji mrejesho wa habari na vipindi vyao.
Hata hivyo wameishukru radio tadio kwa kuona umuhimu wakutembelea vyombo vya habari wanavyofanya navyo kazi na kuwezesha huduma ya radio mtandao.
Nae meneja wa kituo cha radio Baraka Charles Amlike amesema ni fursa kwa kituo chake kwani hiyo itafanya kukitangaza kituo na kumtangaza mwandishi wa habari ambaye ameandika hiyo habari.
Baada ya mafunzo wafanyakazi wakapata nafasi ya kupiga picha ya pamoja na mkufunzi Amua Rushita
Hata hivyo mkufunzi wa mafunzo baada ya kutembelea kituo cha baraka fm Amua Rushita Amesema kumekuwa na mapokeo makubwa ya teknolojia hiyo hali inayofanya vituo vingi kuanza kuvutiwa kujiunga kuwa wanachama katika mtandao wa redio jamii.
Baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku mbili ya TADIO katika hotel ya usungilo jijini Mbeya yaliyoanza septemba 11 na kuhitimishwa septemba 12 mwaka huu shirika hilo limeweka utaratibu wa kuvitembelea vituo wanachama ili kuona namna ambavyo vinafanya kazi na kutumia teknolojia ya radio mtandao.