Vikundi vya usafi vyaomba ushirikiano maeneo wanayofika kufanya usafi
19 September 2023, 12:46
Mazingira ni sehemu yoyote inayomzunguka binadamu na mazingira hayo ili kuepusha athari ikiwemo magojwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu hayana budii kuyalinda kwa kuhakikisha yanakuwa safi wakati wote.
Na Sadoki Mwaigaga
Wafanyabiashara wa soko la Sido jijini Mbeya wameshauriwa kutoa ushirikiano kwa vikundi mbalimbali vinavyofika kufanya usafi eneo hilo ili kuweka mazingira safi muda wote.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Green Awerness Club Winisidasi ambaye amesema suala la usafi ni jukumu la kila mtu hivyo ameomba taasisi na serikali kuwasaidia vifaa vitakavyowasaidia kutekeleza jukumu hilo kwa ukamilifu.
Naye muamasishaji wa Green Awerness Club, Veronika Sanga amewaomba wananchi kushiriki shughuli za usafi hatua itakayo waepusha dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Kwa upande wake afisa Habari wa club hiyo Imani Anyigulile amewaomba viongozi wa serikali kuwahamasisha wananchi kutunza mazingira katika maeneo yao yanayowazunguka.
Aidha mmoja wa wananchi walioshiriki zoezi hilo la usafi Anna mwakajoka amewataka watumiaji wa vyombo vya moto kuacha kutupa au kuambaza taka kwa makusudi kwa kuwa ni kosa kisheria.