Mbeya kuanza kutoa chanjo ya polio kwa watoto chini ya umri wa miaka 8
15 September 2023, 22:46
Wanasema kinga ni bora kuliko tiba,ili uweze kuwa salama huna budii kukubaliana na ushauri wa wataalamu wa afya unaopatiwa juu ya afya yako.kila binadamu tangu kuzaliwa kwake lazima apewe chanjo ili kuweza kuimarisha afya yake, hali hiyo ukiwa kama mzazi au mlezi unapaswa kuilinda familia yako kwa kuwapatiwa chanjo kupitia vituo vya afya vilivyokaribu nawe.
na Hobokela Lwinga
Wazazi na walezi mkoani Mbeya wametakiwa kujitokeza na kuwapeleka watoto wenye umri wa miaka chini miaka 8 kupata chanjo ya Polio inayotarajiwa kutolewa maeneo mbalimbali kuanzia septemba 21-24 mwaka huu.
Akizungumza na kituo hiki afisa chanjo wa jiji Mbeya katika studio za Baraka fm Christopher mathias amesema chanjo hiyo ina umuhimu mkubwa hivyo asiwepo mwananchi wa kupuuzia
Bw.christopher ameongeza kuwa sababu kubwa ya kufanya kampeni hiyo ni kutokana na tanzania kupata mgonjwa katika mkoa wa rukwa .
Aidha afisa chanjo huyo ametaja dalili za ugonjwa wa polio kuwa ni kupata upoozi wa ghafla kwa mtoto pamoja na mtoto kuwa ni legelege huku akisema kila mtu anaweza kupata ugonjwa wa Polio.
Nao baadhi ya wazazi mkoani Mbeya wamesema chanjo hiyo ni muhimu wazazi wote kuhakikisha wanatoa ushirikiano mzuri kwa watakao husika kutoa chanjo hiyo.