Vijana jengeni mazoea ya kumtumikia Mungu na kusoma neno lake
14 September 2023, 18:40
Kanisa ni moja ya taasisi nyeti ambayo ipo katika kuwajenga waumini wake kumjua Mungu na kumtumikia,kutokana na hali hiyo kanisa la Moravian limekuwa na utaratibu wa kuandaa mikutano ya kila idara ili kuwakutanisha waumini kubadilishana vipawa kutokana na rika zao.
Na Rukia Chasanika
Mwenyekiti wa wilaya ya Mbalizi Kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi mchungaji Erika Mwanijembe amewataka vijana kuwa mstali wa mbele kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji na kujifunza neno lake.
Mchungaji Mwanijembe amesema hayo katika mkutano wa vijana kati wilaya ya Mbalizi ulizikutanisha dinari tisa uliofanyika katika kanisa la Moravian ushirika wa Iwindi uliopo mji mdogo wa Mbalizi.
Pichani ni mwenyekiti kanisa la moravian Jimbo la kusini magharibi wilaya ya Mbeya mch.Elika Mwanijembe(Picha na rukia chasanika)
Kwa upande wake Kiongozi wa vijana kati wilaya ya mbalizi kanisa la Moravian bw.Endrew Mwakalinga amesema katika mkutano huo wamejifunza masomo mbalimbali ikiwemo masomo ya uchumba na ndoa ili kuimarisha famila zao.
Baadhi ya vijana walioshiriki katika mkutano huo Elia Kamwela na Tusibwene Mwalwisi katika mkutano huo wamesema mktuano wa mwaka huu umekuwa wa Baraka kwao kwani uimbaji umeimalika kuliko miaka mingine.